Mahakama ya Mwanzo Morogoro kituo cha Ngerengere imetaja kwa mara ya kwanza kesi namba 46 ya mwaka 2025 shtaka la shambulio la kawaida kifungu namba 240 inayomhusu Mwalimu wa Shule ya Msingi Nyambogo anayefundisha madarasa ya awali aliyefahamika kwa jina la Marry Wilbroad John (38) kupigwa na mzazi wa mwanafunzi aliyefahamika kwa jina la Hamisi Kiteu Kashasha.
Akisoma kesi hiyo Hakimu Mkuu wa Mahakama ya mwanzo kituo cha Ngerengere Venance Mwamunyange amesema shauri hilo limetajwa Machi 10,2025 na litasikilizwa tena Machi 20,2025 ambapo mzazi huyo anakabiliwa na mashtaka mawili  shambulio la kawaida kifungu namba 240 kanuni ya adhabu sura ya 16 na shtaka la pili ni kufanya fujo kifungu namba 87 kanuni ya adhabu sura ya 16.
Aidha, Tukio hilo la kushambuliwa kwa mwalimu huyo wa shule ya Nyambogo iliyopo Halmashauri ya Wilaya ya Morogoro lilitokea Machi 3,2025 wakati akiwatoa wanafunzi waliojificha darasani kipindi cha kufanya usafi ndipo fimbo ilimgonga mwanafunzi huyo sehemu ya kiwiko.


 
 
 
 
0 Comments